• KONYAGI

  Konyagi “spirit of the nation” ni kinywaji kongwe kinachoheshimika na kufahamika Afrika Mashariki kote, kwa miaka 40 sasa. Kinywaji hiki kilianzishwa mwaka 1970 kampuni ya TDL ilipoanza kuhamasisha watengenezaji wa pombe za kienyeji kupeleka bidhaa za aina hizo ili ziweze kubadilishwa kuwa vinywaji safi ambazo ni salama kunywa. Ndio hapo ikaanza kuitwa kinywaji safi.

  Konyagi ni bidhaa ambayo imekumbatia utamaduni wake wa Kitanzania. Imetengenezwa kwa kila mtu mwenye umri halali wa kuweza kuinywa. Mpaka sasa, inawakilisha utamaduni, mdundo na mzuka wa Watanzania wote.

 • DRINKING RITUAL

  Konyagi inayo historia ya muda mrefu sana, zikiwemo mila na desturi zake ambazo zimekuwa zikitumika. Moja kati ya hayo ni ufunguaji wa kinywaji hiki.

  Kwanza, mhudumu ataigonga chupa ya Konyagi kwa upande wa chini kutumia kiganja chake mara kadhaa.

  Baada ya kufanya hivyo ndio ataweza kuifungua na kuanza kuimiminia kwenye glasi ya mnywaji huyo.

  Baada ya kumimina chupa inalazwa juu ya meza kwa ubapa wake.

 • MZARAMO

  Unajua nembo hii inamaanisha nini? Ukiachana na uimara wa Konyagi, nembo ya Mzaramo inamuonyesha Mtanzania mwenye nguvu na aliye imara mwenye kujivunia kinywaji chake cha Konyagi!

 • Cocktails
  /sw/cocktails
 • Contact US
  /sw/contact-us
 • Facebook
  https://www.facebook.com/
 • Gallery
  /sw/gallery
 • Heritage
  /sw/heritage
 • Home
  /sw
 • Mzuka
  /sw/mzuka
 • Products
  /sw/products
 • Promotions
  /sw/promotions
 • Sitemap
  /sw/sitemap